The House of Favourite Newspapers

Mambosasa: ”Jambazi Hatari Ameuwawa Dar” – Video

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATIKANA SILAHA MBILI AINA YA BASTOLA NA RISASI 5 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi. Mnamo tarehe 26.09.2019 majira ya saa sita kamili mchana maeneo ya Mbezi Msakuzi njia panda ya Mpiji Magoe zilipokelewa taarifa toka kwa raia wema kuwa kuna majambazi wamepanga kuvamia SACCOSS ya Msakuzi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia Kikosi kazi chake liliweka mtego na ilipofika majira ya saa sita mchana zilifika pikipiki mbili aina ya Boxer ambazo hazikusomeka namba zikiwa na majambazi wanne mmoja kati yao akiwa na bastola.

Majambazi hao walipogundua kama kuna mtego umewekwa walianza kukimbia na ndipo askari walipofyatua risasi hewani lakini hawakusimama na kuanza kujibizana kwa risasi na askari, ndipo askari hao mahili walipofanikwa kuwajeruhi majambazi wawili na majambazi wengine walikimbia kusikojulikana. Aidha majeruhi hao walipopekuliwa walikutwa na bastola moja, risasi tatu ndani ya magazine na maganda mawili ya risasi.

Majambazi hao walipelekwa hospitali na daktari alithibitisha kuwa wameshafariki dunia, miili ya marehemu imeifadhiwa hospitali ya Mwananyamala. Katika tukio la pili, Jeshi la polisi kanda maalum kupitia kikosi kazi chake limefanikiwa kumuua jambazi hatari aliyekuwa anatafutwa kwa muda mrefu kwa kufanya matukio mbalimbali ya mauaji na ujambazi.

Mnamo tarehe 30.09.2019 majira ya saa saba mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipata taarifa kutoka kwa msiri wake kuwa huko maeneo ya Ilala Boma kuna Jambazi sugu anayefahamika kwa jina la EMMANUEL PETER@Mark Silengo akiwa na wenzake wanne wanapanga mipango ya kwenda kufanya uhalifu, kikosi kazi kilifika eneo hilo na kumkuta mtuhumiwa huyo na ghafla akajikuta amezungukwa na askari, ndipo alipotoa silaha yake kwa nia ya kuwafyatulia askari risasi lakini askari walimuwai na kufanikiwa kumjeruhi jambazi huyo na kumnyang’anya silaha aina ya bastola ikiwa na risasi mbili na risasi moja ikiwa chemba imepakiwa tayari kwa kufyatuliwa.

Jambazi huyo alikimbizwa hospitali na wakati akiendelea kupatiwa matibabu alifariki dunia, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.

OPARESHENI MAALUM YA KUKAMATA MAGARI YANAYOPITA KATIKA BARABARA ZA MWENDOKASI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kuanzia tarehe 19/09/2019 lilianza oparesheni maalum ya kukamata magari yanayopita kwenye barabara za Mwendokasi. Katika oparesheni hiyo jumla ya magari 50 yalikamatwa,magari 19 ni mali ya serikali na magari 31 ni ya watu binafsi.

Natoa onyo kwa madereva wa Serikali na madereva wa magari ya watu binafsi kuacha mara moja kupita kwenye barabara za mwendokasi, Jeshi la Polisi linaendelea na oparesheni ya kukamata vyombo vyote vya moto na dereva yeyote atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali za kisheri.

Comments are closed.