Mambosasa: Waliomteka MO ni Wazungu, Tumeweka Vizuzi Wasitoke – Video

KUFUATIA habari za kutekwa  kwa mfanyabishara maarufu nchini ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo) alfajiri ya leo, Oktoba 12, 2018,  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa,  ametoa taarifa za awali kuwa wahusika wanodaiwa kumteka Mo ni watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

Mambosasa amesema kwamba wakati Dewji anafika kwenye gym ya Colosseum eneo la Oyster Bay jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi, kulikuwa na gari moja lililokuwa limefika kabla na kuegesha mbele yake na jingine lilikuwa nje. 

 

Aliendelea kueleza kwamba gari lililokuwa ndani liliashiria kwa kuwasha taa, na lililokuwa nje likaingia ndani na kuegesha mbele ya gari la Dewji ambapo walitoka Wazungu wawili wakambana Dewji na kumuingiza kwenye gari lao aina ya Surf na kuondoka naye kuelekea kusikojulikana.

 

“Tulipopata taarifa hizi Polisi Kanda Maalum tumeanza  kufuatilia mara moja,  na madhumuni ya utekaji huo bado hatujayajua.  

 

“Tukio hili si la kawaida na halijazoeleka, tunafuatilia kwenye mahoteli na maeneo yote, tumeweka vizuizi kuhakikisha watekaji hawa hawatatoka nje ya nchi ili tuweze kuwabana wahuni hawa wanaotoka nje na kuja kuiharibu taswira ya nchi yetu. Waadabishwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

 

“Wananchi wawe watulivu, Dewji lazima apatikane na watekaji watatiwa mbaroni, heshima ya nchi yetu haiwezi kuharibiwa na wageni. Tuendelee kujulishana taarifa yoyote hata kama ni ndogo tutaifanyia kazi,” amesema Mambosasa kwa msisitizo.

 

Baba mzazi wa Mo amesema  taarifa za kutekwa mwanaye zimempa mshtuko na anatumaini Jeshi la Polisi litafanya kazi yake kwa ufanisi zaidi.

BREAKING: MAMBOSASA Anazungumzia Kutekwa kwa MO DEWJI

Loading...

Toa comment