The House of Favourite Newspapers

Mamia Waliofariki kwa Maporomoko, Sierra Leone Wazikwa

0
Uokoaji wa miili ya watu waliofukiwa kwenye maporoko ukiendelea.

 

WIZARA ya Afya nchini Sierra Leone imesema takriban nusu ya maiti 400 zitokanazo na maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa. Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti ya waathirika.

Mafuriko yakitanda baada ya maporomoko.

Lakini Mkuu wa Wataalamu wa Magonjwa kutoka mjini Freetown amesema kwamba baadhi ya mazishi yalikuwa yamefanyika ikiwa ni ya wale ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa. Zaidi ya watu 400 wameripotiwa kufariki dunia tangu kutokana na maporomoko hayo huku 109 wakiwa ni watoto.

 

Vilio na simzanzi.

 

Watu wapatao mia sita mpaka sasa bado hawajulikani walipo kutokana na maporomoko hayo huku Rais wa Sierra Leone akitangaza siku saba za maombolezo nchini humo.

Nathaniel Williams ni daktari katika Hospitali Kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.

Hali ilivyo.

Ameongeza kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.

Leave A Reply