Mamia Wamuaga Rubani Yared Aliyekufa Kwenye Ndege ya Ethiopia

MAMIA ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya mazishi ya kiislam ya rubani mwenye umri wa miaka 29 , Yared Mulugeta Gatechew, aliyekufa katika ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines iliyoanguka Jumapili.

 

Yakijulikana kama sala ya marehemu asiyekuwepo , ibada hiyo ilifanyikakatika msikiti maarufu wa Baluch katika mji wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya Jumanne jioni.

Sala ya marehemu asiyekuwepo imefanyika kuashiria kwamba familia ya rubani wa ngazi ya juu Yared haina matumaini ya kuupata mwili wake, kulingana na mwandishi wa BBC Wazir Khamsin aliyepo mjini Nairobi.

 

Mwanablogi maarufu aliyeko mjini Mombasa alituma video ya ibada ya mazishi huku rubani Capt Yared akionekana upande wa kulia kwake. Rubani huyo wa ngazi ya juu Yared alikuwa na asili ya Ethiopia na Kenya, na baadhi ya ndugu zake wa karibu wanaishi Mombasa, ambako kunatambuliwa kama nyumbani kwa familia yake.

Miongoni mwa watu waliohudhuria sala ya mazishi yake ni mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu nchini Kenya Munir Mazrui na Mkurugenzi wa masuala ya utalii Mohammed Hersi. Mama yake Getachew, Dr Rayan Shapi alikuwa Mkenya wa Mombasa na baba yake Dr Getachew Tessema alikuwa na asili ya Ethiopia. Wazazi wake wanaishi Nairobi.

 

Taarifa zinasema marehemu Getachew ambaye alikuwa na umri wa miaka 29 alisomea masomo ya sekondari katika shule ya sekondari ya Oshwal High mjini Nairobi.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ndege ya Ethiopian airlines Bwana Tewolde Gebre-Mariam, Getachew alikuwa ni rubani wa ngazi ya juu ambaye amekuwa akiiendesha ndege iliyomletea mauti tangu Novemba 2007.

 

Ndege hiyo ilikuwana watu 157 wakiwemo wahudumu wanane waliokuwa waliokuwa wanasafiri kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi na wote walikufa. Wakenya 32 walikuwa miongoni mwao.

Loading...

Toa comment