Man City Yaichakaza Aston Villa
Kocha Steven Gerrard amepokea kichapo chake cha kwanza ndani ya EPL baada ya Aston Villa kulambishwa 2-1 na Manchester City nyumbani Villa Park.
Mabao ya kipindi cha kwanza ya Ruben Dias na Bernardo Silva yametosha kuihakikishia ushindi City na kuendeleza harakati za kutetea taji lake la EPL msimu huu.