The House of Favourite Newspapers

Man Fongo Atoboa Siri ya Kupendwa na Mavenda

ZIKIWA zimepita siku kadhaa tangu kufanyika kwa bonge moja la tamasha lililojulikana kama Tusua Maisha na Global ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live la kuwashukuru mavenda na wasomaji wa Magazeti ya Global, ‘Hitmaker’ wa Ngoma ya Hainaga Ushemeji, Man Fongo ametoboa siri ya kupendwa na mavenda siku hiyo.

 

ILIKUWAJE KWANZA!

Kabla ya Man Fongo kuingia jukwaani ni vema ungejua ilivyokuwa! Tamasha hilo lilikuwa na lengo kuu la kuwathamini na kuwatambua mavenda wote wanaouza Magazeti ya Global Publishers ambayo ni Risasi, Amani, Championi, Uwazi, Ijumaa na Spoti Xtra ambapo umati wa mavenda hao ulikuwepo.

Mavenda waliweza kuongea na uongozi wa Global wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo, Meneja, Abdallah Mrisho pamoja na Mhariri Mtendaji, Saleh Ally. Wauzaji hao walipata nafasi ya kueleza changamoto wanazokutana nazo na kuchukuliwa kufanyiwa kazi.

 

 

KILICHOFUATA SASA

Baada ya kufanya mkutano mfupi wa mavenda, walipata nafasi ya kujumuika pamoja na kupata chakula cha mchana kisha baada ya hapo ilikuwa ni bonge moja la shoo la kibabe.

 

MAN FONGO HUYU HAPA!

Aliyeanza kufungua pazia la burudani mishale ya saa 10:02 Jioni alikuwa ni Man Fongo ambaye aliwaimbisha mavenda ngoma zake zote kali kuanzia Sio Poa na Kujinafasi.

ATOBOA SIRI

Mara baada ya kushuka jukwaani, Man Fongo alitoboa siri ya mavenda kumpenda kwamba wengi wao mbali na kujihusisha na kuuza magazeti ni wapenzi wazuri wa Muziki wa Singeli hasa wake.

“Kama mlivyoshuhudia, karibia wote waliokuja walikuwa wakipenda Singeli na ndiyo maana nilivyoanza tu hamshahamsha kila mmoja aliacha kuendelea kula na kuja kuruka ngoma zangu,” alisema Man Fongo na kuongeza;

“Lakini pia ukiachana na hilo, wauzaji na wasomaji waliokuja wengi wanaimba muziki huu wa Singeli, wapo ninaowafahamu na wengine nimeonana nao hapa, wanaimba Singeli vizuri na huwa wanapanda jukwaani kabisa,” alimaliza Man Fongo.

 

WENGINEO SASA

Baada ya kushuka Man Fongo, burudani ilivamiwa na Mfalme wa Mbagala, Sir Juma Nature a.k.a Kiroboto akiwa na kundi lake la TMK Wanaume Halisi akiwemo, Doro, Rich One, na KR Mullah.

Nature aliwakumbusha mashabiki kwa kupiga nyimbo zake zote zilizotamba kuanzia Sonia, Mgambo, Sitaki Demu, Mtoto Iddi, Mgambo na nyingine kibao.

 

Staa mwingine wa Hip Hop Bongo aliyemaliza shoo alikuwa ni Roma Mkatoliki aliyepanda kwa kuanza na nyimbo yake ya Zimbabwe, Tanzania na Mathematics ambapo aliwafanya mashabiki wengi washindwe kuangalia fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Croatia.

 STORI: MIKITO NUSUNUSU

Comments are closed.