MAN FONGO, MSAGA SUMU WATIFUANA DAR LIVE – PICHAZ

WAKALI wa Muziki wa Singeli Bongo, Man Fongo na Msaga Sumu usiku wa kuamkia leo wametifuana kwa kila mmoja wao kupiga bonge la shoo katika kuadhimisha Sikukuu ya Idd El Fitri ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Katika shoo hiyo iliyoandaliwa na Dar Live, kulishuhudiwa wakali wa kutosha wakipanda jukwaa moja la Dar Live na kuamsha popo mwanzo mwisho.

Shoo hiyo ya kibabe ilianza mishale ya saa mbili kwa wakali hao kupanda huku burudani ya kipekee kwa madensa ikigeuka kivutio kikubwa kwa mashabiki waliohudhuria.

Wakali hao wa Singeli kila mmoja wao alikinukisha mbaya na kusepa na kijiji chake huku wakishangiliwa na mashabiki kuvamia jukwaa mara kwa mara kutokana na kunoga kwa shoo hiyo.

PICHA NA RICHARD BUKOS | Global Publishers.


Loading...

Toa comment