MAN FONGO, SHOLO WATAMBIANA

Sholo Mwamba.

SIKU zikiwa zinah-esa-bika kufikia Aprili Mosi (Sikukuu ya Pasaka), wakali wawili wanaotikisa katika Muziki wa Singeli Bongo, Sholo Mwamba na Man Fongo wameanza kuta- mbiana kufun- ikana kila mmoja katika bonge la shoo la Usiku wa Mwisho wa Ubishi litakalofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Wakizingumza na Star Showbiz kwa nyakati tofauti, Man Fongo alianza kwa kusema kuwa amejipanga vya kutosha kuonesha umwamba wake kwani anaamini katika muziki huo yeye ndiye kinara wanafuata wengine.

 

“Ngoma zangu zote zinajieleza, ukianzia Hainaga Ushemeji, Nani Asiyependa na Safi Tu nadhani utaelewa namaanisha nini.

Niwaombe tu mashabiki wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia nikiwafunika wengine wote ndani ya Dar Live ukumbi wa kijanja,” alisema Man Fongo.

Naye, Sholo Mwamba alisema siku hiyo atahakikisha analiteka jukwaa kwa kutoa shoo ambayo hakuna msanii wa Singeli atakayeweza kuitoa.

 

Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ aliongezea uhondo kwenye shoo hiyo kuwa atakuwepo pia mkali mwingine wa muziki huo, Dulla Makabila ambapo atatoa sapraiz ya aina yake kwa kupanda na mwandani wake, Tiko Hassan ambaye amejiingiza kwenye Bongo Fleva na kuimba naye pamoja kwa mara ya kwanza ndani tangu aanze muziki.

 

“Singeli itakuwa imeteka ukumbi mzima, Dar yote itahamia Dar Live kwa saa kadhaa. Dulla Makabila atahakikisha kila shabiki anacheza na kuimba naye pamoja nyimbo zake zote kuanzia Haujalumba ‘Utatoa Hutoi’, Demu Wako Namba Ngapi pamoja na Makabila,” alisema KP.

KP aliongeza mbali na uwepo wa wakali wa Singeli, kuonesha kuwa utakuwa Usiku wa Mwisho wa Ubishi, katika Muziki wa Taarab napo kutakuwa na makundi yanayotikisa kama vile Yah TMK pamoja na Jahazi Modern.

Man Fongo

 

“Wale wapenda Muziki wa Pwani nayo hii si ya kukosa, Yah TMK itakuwepo jukwaani kuoneshana umwamba na Jahazi Modern chini ya Prince Amigo na niwaambie tu, burudani hii ya mwambao itaanza saa mbili za usiku yaani itakuwa bandika bandua ya burudani mwanzo mwisho kisha wakimaliza tu hawa wa Taarab basi shoo ya kijanja nyingine ya Singeli inaanza hapohapo vyote hivyo kwa mtonyo wa shilingi 7,000 tu getini.”

 

KP alimalizia kuwa mbali na burudani kutoka kwa makundi hayo ya Jahazi na wakali wa Singeli, pia kutakuwepo na burudani ya watoto itakayoanza mapema kuanzia saa mbili za asubuhi huku watoto hao wakipata michezo kibao kama vile kuogelea, kubembea, kuteleza na kucheza na ndege maalum iliopo ndani ya kiwanja hicho cha wajanja ambapo shoo ya watoto itakwenda kwa kiingilio cha shilingi 3,000 tu getini.

“Wananitambua shoo zangu huwa sikwepeshi wala silembi! Watoto wa mama wote kwanza huwa wanasanda. Njoo mwanangu, waite na wana wengine pande zote

STAR SHOWBIZ
Toa comment