Man U, Arsenal Mzigoni Europa Leo
MICHEZO ya hatua ya 32 bora ya Europa League, inatarajiwa kumalizika leo Alhamisi pale ambapo Manchester United na Arsenal zitakuwa nyumbani zikisaka tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Man United wao watacheza pale Old Traff ord dhidi ya Real Sociedad ambapo wana kumbukumbu ya kushinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza, huku Arsenal wakiwa Emirates kuvaana na Benfi ca ambao awali walitoa sare 1-1.
Michezo hii ya leo ndiyo itatoa picha halisi nani kati yao atatinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kwa msimu huu.
Timu nyingine kutoka Premier itakuwa mzigoni leo ni Leicester ambayo awali ilitoa suluhu dhidi ya Slavia Prague, itakuwa nyumbani pale King Power.
Mechi zingine ni Ajax vs Lille, Napoli vs Granada, Rangers vs Antwerp, Shakhtar vs Maccabi Tel Aviv, Hoff enheim vs Molde, Villarreal vs Salzburg, AS Roma vs Braga, Bayer Leverkusen vs Young Boys, Club Brugge vs Dynamo Kiev, Dinamo vs Krasnodar na PSV vs Olympiakos.