The House of Favourite Newspapers

Man U Yaishushia Mvua ya Mabao Leeds Utd, Yaipiga 6-2

0

TIMU ya  Manchester United, jana usiku Desemba 20, 2020,  ilifanikiwa kupata ushindi mzito wa mabao 6-2 dhidi ya Leeds United, kwenye ya mechi za ligi kuu ya England, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Trafford.

 

Huu ni ushindi wa kwanza mkubwa, tangu United walipofanya hivyo dhidi ya Arsenal, msimu wa 2011/12 waliposhinda kwa mabao 8-2 wakiwa chini ya Kocha Sir Alex Ferguson.

 

Magoli ya United yalifungwa na Scotty Mctonmy dakika 2’ na 3’ Bruno Fernandes dakika ya 20 na 69 kwa mkwaju wa penati,  mlinzi wa kati Victor Lindelof  dakika ya 36, na Daniel James 66’.

 

Kwa upande wa Leeds, magoli yao yaliwekwa kambani na Cooper dakika ya 42 na Dallas dakika ya 73.

 

Kocha wa Man United, Ole Gunner Solskjaer, amesema: “Tumeweza kubakiza pointi tatu muhimu nyumbani, hili ni jambo jema na tunapaswa kuwa na muendelezo bora, wachezaji wangu walicheza vizuri na wanahitaji pongezi”.

 

Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford wamesogea hadi nafasi ya ya tatu wakiwa na alama 26 na mchezo mmoja mkononi, Livepool anaoongoza ligi hiyo kwa pointi 31.

Leave A Reply