The House of Favourite Newspapers

Man U Yatayarisha Bn. 77 Kumchukua Pellegrine wa Roma

Lorenzo Pellegrini

Manchester United ya Uingereza wanatayarisha kitita cha Pauni Bil. 26 kumchukua kiungo wa timu ya Roma ya Italia, Lorenzo Pellegrini, mwezi Januari mwaka ujao huku timu yake hiyo ikitia ngumu kutomwachia kirahisi.

Kocha Jose Mourinho wa Man U ambaye ni kipenzi mkubwa wa soka la Pellegrini (22) anayechezea pia  timu ya taifa ya Italia, anataka kumnasa na kumwongeza mshahara wake wa Paundi 890,000 kwa mwaka, kuwa mara mbili; yaani ufikie Sh. bil. 6.7.

Gazeti la michezo la  Italia la Corriere dello Sports, limesema wakala wa Pellegrini aitwaye Giacomo Pocetta, alikutana na wakurugenzi wa United jijini Londoni  ambako klabu hiyo ilipendekeza donge hilo nono.

 

Comments are closed.