Man United Comeback ya Kibabe, Ronaldo Aaamua Mechi

BAADA ya kuanza vibaya katika kipindi cha kwanza na kupigwa bao mbili za chachap, hatimaye Manchester United wanafanikiwa kupindua matokeo kipindi cha pili.

 

Mashetani wekundu,timu ya Manchester United imetoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Atalanta katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

 

Atalanta ilitangulia kwa mabao ya Mario Pasalic dakika ya 15 na Merih Demiral dakika ya 28, kabla ya Man United kuzinduka kwa mabao ya Marcus Rashford dakika ya 53, Harry Maguire dakika ya 75 na Cristiano Ronaldo dakika ya 81.

 

Cristiano Ronaldo akiichezea Man United mechi yake ya 300, anawalaza na viatu Atalanta pale pale Old Traford na kukinusuru kibarua cha kocha wake Ole Guner.

 

Kwa ushindi huo, Man United ya kocha Mnorway, Ole Gunnar Solskjaer inafikisha pointi 6 na kupanda kileleni Kundi F ikizizidi pointi mbili kila moja, Atalanta na Villarreal, wakati Young Boys yenye pointi tatu inashika mkia baada ya mechi tatu.

 

Matokeo hayo huenda yakapunguza presha kwa Mwalimu wa United Ole Gunnar Solkjaer kutokana na kulalamikiwa kutofanya vyema kwa kikosi chake.

 

Man United 3-2 Atalanta

⚽Rashford 53′
⚽Maguire 75′
⚽Ronaldo 81′

⚽Pasalic 15′
⚽Demiral 29′

 

MATOKEO MENGINE

Benfica 0-4 Bayern
Chelsea 4-0 FF Malmo
Lille 0-0 Sevilla
Man United 3-2 Atalanta
Young Boys 1-4 Villareal
Zenit 0-1 Juventus
Salzburg 3-1 Wolfsburg.2179
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment