Man united kukutana na Spurs robo fainali Carabao
Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 pale kwenye dimba la Old Trafford dhidi ya Leicester city, Manchester united iliyo chini ya Kocha wa muda Ruud Van Nistelrooy, itacheza na Tottenham Hotspurs katika hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo.
Jana imeshuhudiwa Man united ikipata ushindi wa mabao mengi zaidi, ukizidi idadi ya mabao yote waliyofunga katika mechi zao nne za mwisho katika michuano yote, kiwango Bora kutoka Kwa Bruno Fernandes aliyefunga mabao mawili, Casemiro aliyefunga mabao mawili pia pamoja na Alejandro Garnacho aliyefunga bao moja, wameifanya Klabu hiyo kupata ushindi mkubwa zaidi msimu huu dhidi ya timu zinazocheza ligi kuu ya Uingereza.
Michuano ya Carabao inatarajiwa kuendelea wiki ya kuanzia Disemba 16, michezo mingine ni Arsenal vs Crystal Palace, Newcastle vs Brentford na Southampton Vs Liverpool, ambapo timu zitakazo fuzu kwenda hatua ya nusu fainali zitakutana kati ya januari 6 mpaka februari 3 na fainali itakuwa Jumapili ya machi 16.
Manchester united siku ya Jumapili Novemba 3, watakuwa pale Old Trafford wakiwakaribisha Chelsea, katika muendelezo wa ligi kuu ya soka ya Uingereza. Chelsea ambao hapo jana wameondolewa katika michuano ya Carabao wako nafasi ya 5 wakiwa na alama 17, wakati Manchester united yuko nafasi ya 14 akiwa na alama 11.