The House of Favourite Newspapers

Man United Kuvunja Mkataba wa Ronaldo Baada ya Kumalizika kwa Kombe la Dunia

0
Nyota wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo

KLABU ya Manchester United ipo katika harakati za kuvunja mkataba wa nyota wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ureno kufuatia kutopendezwa na mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na mwandishi wa Habari Piers Morgan.

 

Katika mahojiano aliyoyafanya Ronaldo ambaye anahesabiwa kuwa moja ya wachezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea duniani, aliishutumu klabu yake hiyo kwa kumsaliti lakini pia kuonesha haina malengo ya kukua baada ya kuwa na umaarufu kwa miaka mingi iliyopita.

 

Aidha Ronaldo alinukuliwa akimshutumu Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Mholanzi Erik Ten Haag kuwa hamheshimu hivyo naye akaamua kutomheshimu.

Manchester United inafikiria kuvunja mkataba wa Cristiano Ronaldo mara baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia

Manchester United kupitia ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii umebainisha kuwa upo katika hatua za awali za kuangalia ni kwa namna gani inaweza kuachana na mchezaji huyo mara tu baada ya kumalizika wka mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchin I Qatar 2022.

 

“Asubuhi ya leo Manchester United imeanza kuchukua hatua za mwanzo kuhusiana na mahojiano ya hivi Karibuni yaliyofanywa na Cristiano Ronaldo. Hatutaoa tamko jingine hadi pale jambo hili litakapofikia hatima.” Ilibainisha taarifa rasmi ya klabu ya Manchester United.

Kwa sasa Cristiano Ronaldo yupo pamoja na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kinachojiandaa kushiriki katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, mashindano yanayoanza kutimua vumbi kesho.

Leave A Reply