The House of Favourite Newspapers

Man United Kuvunja Mkataba wa Ronaldo kufuatia Ukosoaji Wake Dhidi ya Timu

0
Mreno Cristiano Ronaldo.

 

UONGOZI wa Manchester United umeweka wazi kuwa uko tayari kuvunja mkataba wa staa wao, Mreno Cristiano Ronaldo kufuatia ukosoaji wake dhidi ya timu huyo.

 

Ronaldo kupitia mahojiano ya moja kwa moja ya kipindi cha TalkTV cha mwandishi, Piers Morgan alitoa tathmini nzito ya kuhusu Manchester United, huku akiweka wazi kuwa hamheshimu kocha wake, Erik ten Hag.

 

Akizungumza kuhusu hilo rafiki wa karibu wa Ronaldo, Rio Ferdinand alisema: “Huwezi kutetea kile kilichotokea, sioni kama kuna njia yoyote ya kurudi, sihisi kama klabu itamrudisha na wala sidhani kama yeye mwenyewe anataka kurudi. Naamini hii yote imetengenezwa ili aondoke.

 

“Ningeweza kumtetea lakini, kupitia mahojiano haya sioni kama klabu itaruhusu Ronaldo arudi na wakati hamheshimu kocha wao, bila shaka hawawezi. Mapenzi na United yamekwisha. Kitabu kimefungwa ameichafua klabu na hakuna njia ya kurudi.”

Nyota huyo mkongwe alifanya mazoezi na Ureno jana kuelekea Kombe la Dunia, licha ya kukosa mechi mbili za mwisho za United kutokana na kuugua. Ten Hag juzi Jumatatu alikutana na mabosi wa United ili kujadiliana ni maamuzi gani yatafikiwa.

 

United wanaamini kuwa Ronaldo anadhoofisha maendeleo yanayofanywa chini ya bosi wao mpya Ten Hag na umoja alioukuta kambini huku baadhi wachezaji wakionyeshwa kukerwa na staa huyo.

 

Uongozi wa United ulitoa taarifa rasmi ya sakata hilo iliyoeleza: “Kwa sasa lengo letu kuu linabaki kuwa katika maandalizi ya nusu ya pili ya msimu na kuendeleza kasi, imani na umoja unaojengwa kati ya wachezaji, meneja, wafanyakazi na mashabiki.”

 

Chelsea na Sporting Lisbon ni miongoni mwa klabu zinazotajwa huenda zikamsajili Ronaldo ikiwa ataachwa bure na United.

ZITTO ACHARUKA KUHUSU SUK, KIYAMA CHA MADEREVA CHAJA, MASHINE ZA KISASA KUFUNGWA| FRONT PAGE

Leave A Reply