The House of Favourite Newspapers

MAN UNITED VS MAN CITY…NI VITA YA MANCHESTER

  TIMU za Jiji la Manchester, keshokutwa Jumapili zitapambana katika mchezo wa Ligi Kuu England, Premier kwenye Uwanja wa Old Trafford.

 

Timu hizo zitaanza kupambana majira ya saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Michael Oliver, wasaidizi wake ni Gary Beswick na Simon Bennett.

 

Katika msimamo wa ligi hiyo, Man City inaongoza ikiwa na pointi 43, huku Man United inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 35. Tofauti yao ni pointi nane.

Mpaka sasa, Man City ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza hata mechi moja tangu kuanza kwa msimu huu, huku Man United ikipoteza mechi mbili. Man City kutopoteza kwao mchezo mpaka sasa, kunaufanya mchezo huo wa keshokutwa kuwa mgumu zaidi kutokana na uwanja utakaotumika kwani una historia nzuri kwa wenyeji, Man United. Man United ikiwa kwenye uwanja wake huo wa nyumbani, imefikisha mechi 40 bila ya kupoteza.

Inakutana na Man City ambayo katika mechi 15 mpaka sasa za ligi kuu haijapoteza huku pia ikiisaka rekodi ya kushinda mechi ya 14 mfululizo katika ligi hiyo. Hapa kila mmoja anataka matokeo mazuri ili kujiwekea rekodi kivyake. Rekodi za timu hizo katika mechi zao tano zilizopita kwenye ligi hiyo, zinaonyesha kwamba, Man United imekusanya pointi 12 baada ya kushinda mechi nne na kupoteza moja.

 

Wenzao Man City katika mechi hizo, wamekusanya pointi zote 15 kwani walishinda zote tano. Msimu uliopita katika ligi hiyo, mechi ya kwanza ushindi. “United wameonesha kitu fulani katika mchezo uliopita (dhidi ya Arsenal walishinda 3-1) pia watafanya hivyo kwa City.

 

“Nadhani wataifunga City Jumapili, lakini ni bora tukasubiri tuone itakuwaje,” anasema Scholes ambaye alikuwa kiungo hodari wa timu hiyo. Kuelekea mchezo huo, Man City ipo hatihati ya kuikosa huduma ya kiungo wake, David Silva ambaye alipata majeraha kwenye mchezo uliopita wa Premier dhidi ya West Ham United ambapo katika mchezo huo, alifunga bao la ushindi waliposhinda 2-1.

Kocha wake, Pep Guardiola, mpaka juzi alibaki njia panda akiwa hafahamu kama ataweza kumtumia au la kwani alipoulizwa juu ya afya yake, akasema: “Kuna kitu hakipo sawa kwake, aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya West Ham kabla hajafungwa, hivyo sijui kama atacheza.”

 

Wakati Man City ikiwa na wasiwasi wa kumkosa Silva, Man United wenyewe hawatakuwa na huduma ya kiungo wake, Paul Pogba ambaye ana adhabu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Arsenal. Kuhusiana na taarifa za wachezaji wengine wa timu hiyo ambao walikuwa majeruhi kama wataweza kucheza au la, kocha wa kikosi hicho, Jose Mourinho, anasema Nemanja Matic ataanza dhidi ya Man City.

Matic ambaye aliukosa mchezo wa Jumanne ya wiki hii wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow wakati Man United wanashinda 2-1 kutokana na maumivu ya misuli, aliweza kucheza dhidi ya Arsenal licha ya awali kuripotiwa kutokuwa fiti.

 

“Ukweli ni kwamba Eric Bailly hana nafasi ya kucheza, Phil Jones atacheza, Fellaini atacheza, Zlatan ana nafasi kubwa sana ya kucheza na Matic ni majeruhi lakini nakuhakikishieni atacheza. Nawaambia ukweli, Carrick hawezi kucheza,” anasema Mourinho. Hii ni vita ya wababe wawili wa Arsenal ambao wote kwa pamoja walipocheza dhidi ya timu hiyo msimu huu, waliibuka na ushindi unaofanana wa mabao 3-1. Ni muda wa kusubiri na kuona dakika tisini zitaamua nini.

Comments are closed.