Kartra

Man United Yabanwa England, Harry Kane Arejea na Ushindi Spurs

MANCHESTER United wakiwa ugenini jana walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton.

 

Huu ulikuwa mchezo wa pili wa Ligi Kuu England baada ya timu hiyo kuwika kwenye mchezo wa kwanza wa ligi, lakini jana walikuwa kwenye wakati mgumu.

 

Mason Greenwood, alifanya kazi kubwa ya kwasawazishia United baada ya Fred kujifunga mwanzoni na kuanza kuleta taharuki.

 

United ambao mchezo wa kwanza waliwachapa Leeds mabao 5-1, jana walionekana kuwa kwenye wakati mgumu sana ambapo Southampton walitawala mchezo kwa sehemu kubwa.

 

Kinda wao mpya Jadon Sancho, aliingia kipindi cha pili lakini bado alishindwa kuwasaidia, huku United ikimweka nje Rafael Varane ambaye amesajiliwa kutoka Real Madrid.

 

Mchezo mwingine wa jana mapema uliwashuhudia Spurs wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wolves, bao lao pekee likifungwa na Dele Alli kwa mkwaju wa penalti.

 

Huu ni mchezo wa pili Spurs anashinda baada ya kuibuka tena na ushindi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Man City. Harry Kane, ambaye awali aligoma akishinikiza kuuzwa aliingia kwenye mchezo huu dakika 19 za mwisho na ilibaki kidogo sana aifungie timu yake bao la pili.

Manchester, England


Toa comment