Man United Yaibana Chelsea

Vinara kunako Ligi ya EPL, Chelsea wamepunguzwa kasi baada ya sare ya 1-1 na Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London usiku wa Jumapili.

 

Katika mchezo huo ambao Chelsea waliutawala kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo mpaka ya mwisho, ulionesha namna kocha wa sasa Michael Carrick alivyowekeza katika mbinu za kujilinda pindi anapokutana na timu yenye makali kuliko yeye.

 

Jadon Sancho alianza kuifungia Manchester United dakika ya 50, baada ya uzembe wa Kiungo wa Chelsea Jorginho kushindwa kutuliza mpira kwa umakini, hilo likiwa bao lake la pili wiki hii, kabla ya Jorginho kuisawazishia The Blues kwa penalti dakika ya 69 kufuatia Aaron Wan-Bissaka kumchezea rafu Thiago Silva.

 

Mlinda mlango wa Man United, David De Gea alifanya kazi kubwa kuokoa hatari langoni mwake na kuhakikisha angalau wanaambulia alama 1.

 

Chelsea inafikisha pointi 30 baada ya sare hiyo na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi mbili zaidi ya Manchester City, wakati Man United inafikisha pointi 18 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi 13.702
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment