The House of Favourite Newspapers

Man United Yajiaminisha Kumsajili Sancho

0

KLABU ya Manchester United inaamini ipo katika nafasi nzuri ya kufanikisha dili la kumsajili winga Jadon Sancho kwa ada ya pauni 120m mwishoni mwa msimu huu.

 

Nyota huyo wa Borussia Dortmund amekuwa akitajwa kuwa njiani kuondoka klabuni hapo, tayari klabu kadhaa kubwa zimetajwa kumuwania lakini United inapewa nafasi kubwa ya kumsajili.

 

Sancho alijiunga na Dortmund akitokea kwa wapinzani wa jadi wa United, Manchester City mwaka 2017. Klabu nyingine ambazo zinatajwa kumuwania ni Liverpool, Chelsea, Barcelona na Juventus.

Dau la pauni 120m linatajwa kuwa ni kubwa kuliko ambalo limewekwa mezani na timu nyingine zote ambazo zinamuwania, ndiyo maana wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili.

 

Ikiwa United itakubali kutoa dau hilo itakuwa imevunja rekodi yake ya kumsajili mchezaji kwa gharama kubwa zaidi, anayeshika rekodi hiyo klabuni hapo ni Pau Pogba aliyesajiliwa kwa pauni 89m akitokea Juventus.

 

Sancho amefunga mabao 16 msimu huu katika michuano yote kabla ya michezo kusimama.

 

Leave A Reply