Kartra

Man United Yamtaka Harry Kane

BOSI wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajer amekiri kuwa anahitaji kusajili straika (Harry Kane), licha ya kumuongezea mkataba Edinson Cavani.

 

Wiki hii, Harry Kane ametangaza kuwa anataka kuondoka ndani ya Tottenham kwenda kusaka changamoto mpya na kusaka mataji.

 

Man United, Man City na Chelsea ndiyo zinatajwa kuwania saini ya straika huyo. Solskajer alisema anahitaji kujenga kikosi chake kwa kuhakikisha anasajili straika.

 

“Unajua siwezi kuwazungumzia wachezaji wa timu nyingine (Kane) sababu sipaswi kufanya hivyo, ila nitasajili straika.“Tunahitaji kuwa na kikosi imara na kilicho bora. Na tunatakiwa kuangalia vitu vingi mpaka kutengeneza aina ya kikosi hicho.

 

“Sisemi kuwa kama Edi (Cavani) anabaki hivyo siwezi sajili straika mwingine hapana. Edi amesaini, ila unajiuliza una mastraika wangapi ndani ya kikosi? Hivyo siwezi sema sitasajili straika wakati nataka kujenga kikosi bora.


Toa comment