Man United Yasajili Mashine Mpya

WINGA mpya wa Manchester United, Amad Diallo, amewatumia ujumbe wa hisia kali mashabiki wa timu yake ya zamani, Atalanta, kufuatia kukamilisha uhamisho wake Old Trafford.

 

Winga huyo, 18, amekamilisha usajili wake Manchester United kwa pauni milioni 37 kwa mkataba wa miaka minne na nusu, juzi Alhamisi.

 

Mashetani hao Wekundu wamelipa pauni milioni 19 keshi lakini dau hilo linaweza kuongezeka kwa ziada ya pauni milioni 18 kutegemea na atakachokifanya uwanjani.

Diallo ambaye ameichezea Atalanta mechi tano tangu aibukie kwenye akademi ya klabu hiyo, juzi aliandika kwa hisia kali: “Wapendwa Atalanta, muda wa kusema kwaheri umewadia. Imekuwa ni miaka sita ya ajabu, miaka sita ya kukua, miaka sita ya changamoto.

 

Lakini muhimu zaidi, miaka sita ya furaha na upendo. Hapa, nimekuwa mwanamume, mmenipa kila kitu nilichotaka, na ninajivunia sana kuwahi kuichezea Atalanta.

 

Daima mtakuwa na nafasi kwenye moyo wangu. Popote nitakapoenda, mtakuwa pamoja nami, sasa na daima!”Kinda huyu alifuzu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi juzi lakini alisajiliwa na United katika usajili uliopita Oktoba kisha akabaki kwa mkopo Italia katika nusu ya kwanza ya msimu.

 

Akimzungumzia kinda huyo, Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer, alisema: “Kama klabu, tumemfuatilia Amad kwa miaka mingi na baada ya kumuangalia mimi binafsi, naamini ni mmoja wa vipaji vya kuvutia katika soka.

Ni mchezaji mwenye vigezo vyote vinavyohitajika kuwa mchezaji muhimu kwa Manchester United.”Tecno


Toa comment