The House of Favourite Newspapers

Man United Yatinga Fainali Europa Kibabe

0

  

Manchester, Uingereza

HATIMAYE sasa fainali  ya Kombe la Europa ni  Manchester United dhidi  ya Ajax mjini Stockholm kwenye  Uwanja wa Friends Arena, Mei 24. United na Ajax zimefuzu kwenye fainali  hiyo baada ya kuchomoza na matokeo  mazuri, jana.

United ambao walikuwa kwenye Uwanja  wa Old Traff ord kuvaana na Celta Vigo  walifanikiwa kuchomoza na sare ya bao  1-1, lakini wakafuzu kwa fainali baada ya  kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza  nchini Hispania wiki moja iliyopita.

Huu ulikuwa ushindi muhimu kwa kocha wa United Jose Mourinho, ambaye alishasema kuwa anachotazama sasa ni kutwaa ubingwa huo ili aweze kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, kwa kuwa ameshaona kuwa hawezi kupata nafasi ya kumaliza kwenye nne bora nchini England.

Hata hivyo, katika dakika ya 86, mchezo huo ulichafuka baada ya Roncaglia wa Celta Vigo na Eric Bailly wa United, kupewa kadi nyekundu kutokana na kusukumana.

Celta Vigo, ambao walisafi ri kwenda England na zaidi ya mashabiki 3,000, walianza mchezo huo kwa kasi ya hali ya juu na kuonyesha matumaini kuwa wanaweza kupata bao la mapema, lakini mambo hayakuwa hivyo.

Katika dakika ya 17 ya mchezo  walikumbana na mlima mrefu baada ya kiungo wa United, Marouane Fellaini kuifungia timu yake bao pekee kwenye mchezo huo kwa kichwa safi akimalizia pasi iliyopigwa na Marcus Rashford.

Hili lilikuwa bao la kwanza kwa kiungo huyo baada ya kucheza michezo 10 ya michuano hiyo msimu huu.

Baada ya kufungwa kwa bao hilo hakukuweza kuwapunguza nguvu Wahispania hao, kwani waliendelea kucheza kwa kasi ya hali ya juu na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao.

Hata hivyo, juhudi zao zilizaa matunda katika dakika ya 85 baada ya Roncaglia kuwasazishia bao hilo na kuwapa presha kubwa United, lakini dakika chache mbele akala kadi nyekundu.

Mshambuliaji wa Celta, Iago Aspas, alionyesha uwezo mzuri kwenye mchezo huu lakini alikosa nafasi nyingi sana za wazi.

Kama Mourinho atachukua ubingwa huu itakuwa mara yake ya kwanza kuchukua kombe hilo la pili kwa ukubwa baada ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Endapo United watatwaa ubingwa huu basi wataweka kibindoni kitita cha Euro milioni 6, ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 15.

Manchester United haijawahi kutwaa ubingwa huu na kama itautwaa basi itakuwa rekodi ya kwanza kwenye timu hiyo.

Timu za England ambazo zinaongoza kwa kutwaa ubingwa huo ni Liverpool waliotwaa mara tatu na Tottenham Hotspur mara mbili.

Katika mchezo mwingine, Ajax ambao walipata ushindi wa mabao 4-1 nyumbani kwao dhidi ya Lyon kwenye mchezo wa kwanza, jana walichapwa mabao 3-1 nchini Ufaransa, lakini wakatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4.

Ajax ambao wametwaa ubingwa huu mara moja, imekuwa timu tishio kwa msimu huu ikiwa na wachezaji wengi chipukizi.

Dolberg alikuwa wa kwanza kuwafungia Ajax katika dakika ya 27, lakini Lacazette alitumia dakika moja tu kuwafunga mabao mawili, ambapo la kwanza alifunga katika dakika ya 45 na la pili dakika moja ya nyongeza kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza kwenye Uwanja wa Lyon – Decines .

Katika dakika ya 81, Ghezzal, aliifungia Lyon bao safi na kuanza kuwapa presha ya juu Ajax, ambao walipambana hadi mwisho na kupata faida ya ushindi wa mchezo wa kwanza.

LIVE: Salum Mkemi Amfungukia Ngoma, Yanga Kukosa Uwanja wa Mazoezi

Leave A Reply