Kartra

Man Utd Kukinukisha Fainali ya Europa leo Usiku

FAINALI ya 50 ya michuano ya UEFA Cup/UEFA Europa League pia ni msimu wa 12 tangu itoke kuitwa UEFA Cup na kuwa UEFA Europa League.

 

Mchezo huu utazihusisha timu kutoka Hispania, Villarreal na ile ya England, Manchester United na unatarajiwa kupigwa saa 4:00 usiku ikiwa ni siku chache kabla ya fainali ya UEFA Champions League kupigwa na kumaliza michuano ya Ulaya kisha kuelekea kwenye UEFA EURO 2020 itakayoanza Juni 11, mwaka huu.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa Villarreal kutinga fainali ya michuano ya Ulaya, timu hii haijawahi kushinda taji lakini walifanikiwa kumaliza wa pili kwenye michuano ya UEFA Intertoto Cup mara mbili mwaka 2003 na 2004.

Hata hivyo kocha wao, Unai Emery ana rekodi nzuri kwani hii ni mara ya tano anacheza fainali ya UEFA Europa League; ameshinda mataji matatu tena mara tatu mfululizo akiwa anakinoa kikosi cha Sevilla, alibeba mwaka 2014, 2015 na 2016, kabla ya kupoteza mwaka 2019 akiwa na Arsenal.

 

Manchester United itacheza fainali yao ya pili ya UEFA Cup/Europa League, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2017 na ilichukua taji.

 

Kwa ujumla hii ni mara ya nane kucheza fainali za michuano ya Ulaya.Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjær anacheza fainali ya kwanza tangu akiwa kocha wa klabu, kumbuka aliwahi kufunga bao la ushindi akiwa na United mwaka 1999 katika fainali ya UEFA ni kama miaka 22 imepita hadi sasa.

 

Timu hizi zimekutana mara nne kwenye hatua ya makundi ya Uefa kati ya msimu wa 2005–06 na 2008–09 na michezo yote ikaisha suluhu.

 

Bingwa atapatiwa kombe na washindi wa pili watapata medali ambapo zimeandaliwa 40 kwa wachezaji na stafu wengine na watakapokuwa wanakabidhiwa hawataruhusiwa kushikana mikono.

 

Substitutions tano hadi sita zitaruhusiwa kama wataenda hadi dakika za nyongeza.Iko hivi, mechi itapigwa dakika 90 ikiwa sare zitaongezwa dakika 30 pia ikiwa sare ndipo itapigwa mikwaju ya penalti.


Toa comment