Man Utd Yaichinja Chelsea, Yaipiga Bao 4-0, Rashford Atupia 2 – Video

Marcus Rashford

MANCHESTER United imeanza vema msimu huu wa Ligi Kuu England ‘Premier League’ baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Chelsea, jana Jumapili.

 

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford nyumbani kwa Manchester United, ulianza kwa kasi huku Chelsea ikionekana kufanya mashambulizi ya mapema lakini baadaye kibao kiligeuka na kuwafanya Chelsea kutoamini kilichotokea.

 

Dakika ya nne tangu kuanza kwa mchezo huo, Tammy Abraham wa Chelsea alipiga shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari la Manchester United na mpira kugonga mwamba wa pembeni kisha kurudi uwanjani.

 

Baada ya shambulizi hilo, Manchester United wakatulia na kuanza kushambulia kwa kushtukiza ambapo dakika ya 17, beki wa Chelsea, Kurt Zouma, alimchezea vibaya Marcus Rashford akiwa ndani ya eneo la hatari na kusababisha penalti.

Penalti hiyo ikafungwa na Rashford na kuifanya timu yake Manchester United kuwa mbele kwa bao moja hadi mapumziko. Safu ya ulinzi ya Man United ilikuwa ikiongo zwa na bei wao mpya ambaye ni ghali kuliko wote katika rekodi ya usajili kwa walinzi duniani, Harry Maguire ambaye alionyesha uwezo mzuri.

 

Kipindi cha pili Manchester United walirudi kwa kasi kwani muda mwingi walikuwa wakilishambulia lango la Chelsea ambapo mashambulizi hayo yalizaa Lampard.

Awali, kabla ya mchezo huo, mapema ilishuhudiwa Arsenal ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa St. Jame’s Park, iliwafunga wenyeji wao, Newcastle United bao 1-0 lilofungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 58, huku Leicester City ikishindwa kufungana na Wolverhampton Wanderers.

MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): de Gea, Wan Bissaka, Maguire, Lindelof, Shaw, McTominay, Pogba, Andreas Pereira (James 74), Lingard (Mata 85), Martial, Rashford (Greenwood 85);

SUBS NOT USED: Young, Romero, Matic, Tuanzebe

SCORERS: Rashford (18, 67), Martial (65), James (81)

BOOKED: Lingard, Lindelof

CHELSEA (4-2-3-1): Arrizabalaga, Azpilicueta, Christensen, Zouma, Emerson Palmieri, Jorginho (Kante 73), Kovacic, Pedro, Barkley (Pulisic 58), Mount, Abraham (Giroud 66);

SUBS NOT USED: Alonso, Caballero, Kenedy, Tomori

SCORERS: NONE

BOOKED: Zouma, Abraham, Kante


Loading...

Toa comment