Man Utd Yatupwa Kwa Barcelona, Robo Fainali UEFA

BAADA ya kufanya ‘comeback’ ya hatari dhidi ya PSG, sasa Manchester United imepangwa kukutana na kigogo mwingine kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kigogo huyo ni Barcelona, ambao ni mabingwa wa zamani wa michuano hiyo wanaoongozwa na Lionel Messi, na sasa wanapewa nafasi kubwa ya kutinga nusu fainali kutokana na matokeo yao ya hivi karibuni.


Tangu kuondoka kwa kocha Alex Ferguson mwaka 2013, United imekuwa ikipata wakati mgumu na kusababisha kufukuza makocha kadhaa, hivyo kupangwa kukutana na Barcelona ni mtihani mgumu kwa kocha wa muda wa sasa
kikosini hapo, Ole Gunnar Solskjaer.

 

Hatua hiyo inashirikisha timu nane, nne kati ya hizo ni kutoka England, ambapo Tottenham watakuwa wenyeji wa Manchester City huku Liverpool wakipa- ngwa kukutana na FC Porto. Kukutana baina ya Man United na Barcelona ni kumbukumbu ya michuano hiyo ya mwaka 2009 na 2011 ambapo mara zote Barcelona ilishinda. Mshindi wa mchezo wa United na Barcelona anatarajiwa kukutana na mshindi wa mechi ya Liverpool na Porto.

 

Upande mwingine, Ajax baada ya kuwatoa mabingwa watetezi, Real Madrid, wamepangwa kukutana na
Juventus ambao wanaongozwa na Cristiano Ronaldo. Mshindi wa mchezo wa Tottenham na Man City atakutana na mshindi wa mchezo wa Ajax dhidi ya Juventus. Michezo ya kwanza ya hatua hiyo inatarajiwa kuanza Aprili 9 na 10, kisha marudio ni Aprili 16 na 17, mwaka huu.

Toa comment