The House of Favourite Newspapers

SIMBA VS MBABANE FC, MANARA Ataja Viingilio – Video

MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kuhusu maandalizi ya mechi yao ya Kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows FC ya nchini Swaziland, na kudai kuwa wamepokea taarifa kutoka TTF tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kutimua vumbi keshokutwa November 28 , 2018 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na vyombo vya habari jijini dar es salaam leo, Manara amesema; “Tunakwenda kuwakabili Mbambane keshokutwa jumatano tukijua ni Timu nzuri na mabingwa wenzetu,bt tunajua matarajio ya Watanzania na Wanasimba kwetu,kiukweli hatutawaangusha na tunaahidi furaha kwenu.
Viingilio ni ;

5,000
7,000
10,000 
20,000

‘Tukutane Uwanja wa Taifa Saa kumi alasiri Tarehe 28/11/2018 ,Tunawaomba Watanzania na Wanasimba tuujaze uwanja na kuwapa nguvu wachezaji wetu.”

Mbabane Swallows FC tayari wamemewasili nchini leo usiku huku akijinasibu kuwa wamejipanga vyema kuikabili timu hiyo.

VIDEO: MSIKIE MANARA AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.