The House of Favourite Newspapers

MANARA Amwaga POVU, Amfananisha CHAMA NA INIESTA – Video

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Clatous Chama, ameendelea kudhihirisha moto kwa kuweza kutumia akili na kasi uwanjani leo katika mchezo wa marudiano wa ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa katika uwanja wa Mavuso Sports Center Manzini nchini Eswatini.

 

Simba imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo iliyopigwa ugenini, hivyo kufanya jumla mabao yawe 8-1.

 

 

Chama amefanikiwa kumrudisha nyuma ya nyavu mlinda mlango wa Mbabane dakika ya 27 na 32 kwa kuutendea haki mpira uliopigwa na Emmanuel Okwi, dakika ya 32 Okwi naye akatupia dakika ya 51 na Kagere akatupia dakika ya 62 .

 

Kwa matokeo hayo Simba wanafanikiwa kufikisha idadi ya mabao 8-1 na kufanikiwa kusonga mbele katia hatua ya kwanza. Mchezo umemalizika, ambapo kipindi cha kwanza Mbabane walifanya mabadiliko ya wachezaji wawili na wachezaji wao wawili walipewa kadi ya njano kutokana na kuwachezea rafu wachezaji wa Simba.

Comments are closed.