Manara Azungumzia Yanga Kupangiwa Mechi 7 Taifa

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara.

OFISA Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema klabu yake haioni tatizo lolote kuhusu mechi saba za ligi kuu ambazo klabu ya Yanga itacheza katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ratiba inaonyesha kuwa katika mechi 11 zijazo za Yanga, itachezea uwanja huo, nne zikiwa za ugenini.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Manara amsema endapo ratiba kama hiyo ikija kupangwa upande wao, Yanga isilalamike kwa kusema viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ni wapenzi wa Simba.

Alichokisema Haji Manara kupitia page yake ya Instagram:-

”Haijawahi kutokea kokote duniani toka Ulimwengu umeumbwa!! Klabu moja kucheza mechi 12 mfululizo kwenye kituo chake..usisahau JKT,Simba,kMC na Lyon zitachezewa Taifa,,
Hoja hapa ni nn?jambo hili lingekuwa kwetu Gongowazi wangesema TFF hii ni Simba,na cc hatulalamiki tunakumbushana tu…
Hata hili la kufungiwa Meneja wetu ingekuwa wao wangehoji why Meneja wao hajafungiwa ?wakati makosa ya kina kichuya ndio aliyoyafanya Toto?
Soma bila jazba utanielewa nimemaanisha nn!!
Narudia hatulalamiki ila isije tokea kwetu halaf nisikie fyoko fyoko..Ndegelec!!”

Loading...

Toa comment