Manara Avunja Ukimya Baada ya Kukosa Tuzo

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kubwagwa kwenye tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) msimu wa 2020/21, kipengele cha Muhamasishaji Bora.

Tuzo hiyo ilikwenda kwa shabiki kindakindaki wa Taifa Stars, Nick Renold maarufu kama Bongo Zozo, ambaye aliwashinda Manara na Masau Bwire wa kKlabu ya Ruvu Shooting.

Manara amefunguka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, akimjibu Bongo Zozo ambaye amesema wazi kwamba hakustahili kutangazwa kuwa mshindi na iwapo yeye ndiyo angekuwa anatoa tuzo hiyo, angempa Manara.

Bongo Zozo anaamini Manara alistahili tuzo hiyo kwa kazi kubwa ya kuwahamasisha Mashabiki aliyoifanya kwa timu ya Taifa Stars na alipokua Simba SC kabla ya kuhamia Young Africans.

Manara Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika: “TFF wanajua mm na ww ni marafiki na majirani hapa Dar.. ukiishi Sleep Way jirani na kwangu, ndio maana hata kadi yako ya jana ya mwaliko ililetwa kwangu.”2177
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment