Manara Avuruga Mashabiki Unguja

BAADHI ya mashabiki wa mpira wa miguu Unguja wamesema msimu wa 2021-2022 wa Ligi Kuu Bara hautakuwa na msisimko mkubwa kutokana na kung’atuka kwa aliyekuwa msemaji wa Simba Sc, Haji Manara.

 

Haji Bakari Haji, shabiki wa Yanga alisema: “Japo Manara alikuwa akitukera na baadhi ya kauli zake, lakini alikuwa anachangamsha sana ligi hususan zikikutana timu mbili Simba na Yanga,”

 

“Zile kauli za Manara zilikuwa zinawafanya wachezaji wetu wapambane kweli, lakini sasa hivi hayupo sijui msimu unaokuja itakuwaje, ila tutammisi,”

 

Ali Juma na Haji Issa ambao ni mashabiki wa Simba walisema walikuwa wakivutiwa na kauli za Manara hususan akiwa anawatania watani zao, Yanga.

 

“Hakuna binadamu ambaye hana upungufu hata Manara anayo yake, lakini kwenye usemaji aliitendea haki Simba hata ukisikiliza vipindi vya redio vya michezo siku ambayo kuna sauti yake vinanoga kweli, lakini hatuwezi kupinga kilichotokea,” alisema Ali.

 


Toa comment