Kartra

Manara: Ingekuwa ‘Fair’ Yanga Ingeshuka Daraja

AFISA Habari wa klabu ya soka ya Simba SC Haji Manara amesema kwasasa ubora wa wachezaji wa Simba SC ni mkubwa sana ukilinganisha na wachezaji wa Yanga SC ambapo amedai kama kungekuwa na usawa Yanga ingeshuka daraja.

 

Manara ameyasema hayo leo kupitia East Africa Radio alipokuwa akiongea mchezo wa watani wa jadi Jumamosi Mei 8, 2021.

 

”Ukitazama wachezaji wa Yanga SC kama kungekuwa na fair wangeshuka daraja, kwasasa wapo nafasi ya pili ni kwasababu ya ukubwa ukubwa tu lakini hawana ubora wa kuifikia Simba SC, iko mbali sana,” amesmea Haji Manara.

 

Aidha Manara ameongeza kuwa wamejipanga kuwafunga Yanga SC na kuchukua ubingwa kabla ya mechi 5 ligi kumalizika kisha wakapambanie ubingwa wa Afrika kwenye klabu bingwa.

 

”Kwanza tunaanza kumfunga Yanga SC kisha tunachukua ubingwa kabla ya mechi 5 ligi kumalizika kisha tunaenda kushughulikia kombe kubwa Afrika. Hakuna mjadala huu ubingwa wa Tanzania tunachukua miaka 10 mfululizo,” ameeleza.

 

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja na Global Radio kuanzia saa 10:00 jioni ambapo utafanyika uchambuzi kabla ya mechi, matangazo ya dakika 45 za kwanza, uchambuzi wakati wa mapumziko, dakika 45 za mwisho na uchambuzi baada ya mechi.


Toa comment