Manara Kuishitaki Simba Sc

Msemaji wa Klabu Yanga Haji Manara amesema anakwenda kuwashitaki waajiri wake wa zamani, Klabu ya Simba kwa kumtumikisha bila mkataba.

 

“Naenda Mahakamani kuwadai fidia simba wamenitumikisha bila mkataba, na nataka iwe fundisho kwa Taasisi zote zinazoajiri watu na kuwatumikisha bila mikataba.┬áNitaenda mahakamani kudai haki yangu, nawadai Simba pesa nyingi, wamenitumikisha miaka zaidi ya 6.

 

“Nimefanyiwa dhuruma, hawa sio binadamu na kwakweli mimi nina kifua Sijawahi kusema ila siku nikisema mtanielewa, kisa umaarufu eti mtu ananichukia.┬áNa iliwauma zaidi mimi kwenda Yanga, walinifanyia mambo mengi mabaya, nitadai haki yangu, nimeaanda mawakili 10,” amesema Manara.


Toa comment