The House of Favourite Newspapers

Manara: Tunashusha Sapraiz la Kidunia

0

UONGOZI wa klabu ya Yanga umezidi kuchimba mkwara kuwa lolote linaweza kutokea kwenye nafasi mbili za kusajili nyota wa kimataifa walizosaliwa nazo, ambapo wamepanga leo Ijumaa au kesho Jumamosi kutingisha tena kupitia usajili.

 

Yanga mpaka sasa wamekamilisha usajili na kuwatambulisha wachezaji wapya kumi kwa ajili ya msimu ujao, ambapo kwa nyota wa kimataifa bado wamesaliwa na nafasi mbili za kusajili.

 

Kuhusiana na masuala ya usajili, Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kuhusu wiki ya Mwananchi kila kitu kipo vizuri, mashabiki watarajie makubwa ambapo kesho wachezaji waliosalia Morocco wataingia, lakini niwakumbushe kuwa bado tuna nafasi mbili za nyota wa kimataifa.

 

“Hatutaki kulizungumzia hili lakini lolote linaweza kutokea, kesho au keshokutwa tutatingisha tena tumefanya hivyo kwenye tasnia ya habari kwa kumvuta Manara, tutafanya hivyo tena kwa wachezaji.”

 

Akizungumzia mipango ya Yanga msimu ujao, msemaji wa klabu hiyo Haji Manara alisema: “Tunatengeneza kikosi ambacho kitarejesha kila kombe kuanzia msimu ujao, hatutalalamika tena, Nugaz na Bumbuli kwenye hamasa walifanya kazi kubwa kuna eneo nitajaribu kuliongezea nguvu hasa kwenye kujiamini kwa mashabiki.

 

“Hatuhitaji kulalamika kwa usajili tulionao, Yanga ni kubwa mno hatutakiwi kuwa wanyonge, Afrika Mashariki na Kati hakuna
anayetufikia.

 

SABABU ZA KUONDOKA SIMBA
“Vilifanyika vitu vingi
hasa kampeni chafu ya kuharibu maisha yangu na ‘brandi’ yangu, lakini kilichoniumiza zaidi ni
kuniita msaliti, kama
wakithibitisha kuwa mimi ni msaliti hata kwa asilimia moja basi naachana na mpira.

 

KUHUSU WIKI YA MWANANCHI
“Tunalokwenda kufanya
halijawahi kutokea, leo tunazindua nyimbo ya Yanga ambayo imeimbwa na Nandy
na nikuhakikishie
kuwa mpaka sasa kuna kundi kubwa la wasanii wakubwa wakike, na wakiume ambao wameomba kuingia nami siku hiyo.“Lakini pia tutakuwa na Koffi Olomide ‘Mopao’ na pia tutakuwa na ‘Sapraizi’ ya kidunia.

 

ISHU YA GERALD MDAMU
“Kama sehemu ya wadau
wa soka, tumejipanga kuchangia kitu ambapo sisi Yanga kupitia mdhamini wetu bosi Ghalib Said tutachangia kiasi cha Shilingi 6,700,000.

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam

MAUAJI DAR MAPYA YAIBUKA, ALIWAHI KUJIRUSHA TOKA GHOROFANI|BUNGE LATAKA SLAA AKAMATWE


Leave A Reply