The House of Favourite Newspapers

Mangungu, Kaluwa Ngoma Nzito Simba, leo Jumapili Kufanya Mkutano Mkuu

0

KLABU ya Simba, leo Jumapili inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wenye ajenda 13 ikiwemo ishu ya uchaguzi mkuu wa kuchagua mwenyekiti na wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi.

Katika uchaguzi huo, wanaowania nafasi ya mwenyekiti ni Murtaza Mangungu anayetetea kiti chake na Moses Stewart Kaluwa.

Wajumbe wanaochuana ni Seif Ramadhan Muba, Seleman Harub Said, iddi Halifa Kitete, Issa Masoud Iddi, Abubakar Zebo, Abdallah Rashid Mgomba, Elisony Edward Mweladzi, Rashid Mashaka Khamsini, Rodney Makamba Chiduo, Aziz Mohamed, Asha Baraka na Pendo Aidan Mapugilo.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Dar, kuanzia saa 2 asubuhi.

Ajenda 13 za mkutano huo zitakuwa hivi; 1. Kufungua mkutano, 2. Kuhakiki idadi ya wanachama waliohudhuria mkutano, 3. Kuthibitisha ajenda, 4. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita, 5. Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita, 6. Hotuba ya mwenyekiti, 7. Kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kutoka Bodi ya Wakurugenzi.

Zingine ni; 8. Kupokea taarifa za hesabu zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia za Simba Sports Club na Simba Sports Club Company Limited, 9. Kupokea bajeti ya mwaka ya shughuli na mipango ya Simba Sports Club na Simba Sports Club Company Limited, 10. Uchaguzi wa nafasi zote zilizowazi za Simba Sports Club na Simba Sports Club Company Limited, 11. Kupokea na kujadili mapendekezo ya marekebisho ya kanuni na katiba za Simba Sports Club, 12. Kujadili mapendekezo yaliyosawilishwa na wanachama au Bodi ya Wakurugenzi, 13. Kufunga mkutano.

MAZIKO ya SHEMEJI wa BERNARD MEMBE, KABURI LAFUKULIWA WAZIKWA SEHEMU MOJA na MUMEWE…

Leave A Reply