The House of Favourite Newspapers

Manispaa ya China Kushiriki Maendeleo ya Wilaya ya Ilala, Dar

mama-mjema-1

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akiwa kwenye mkutano na wawakilishi kutoka China. Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko.

mama-mjema-2Mwakilishi kutoka nchini China wa pili kutoka kushoto ni Zhang Aijun (wa pili kushoto) akiongea katika hafla hiyo, akiwa na wajumbe wenzake.

mama-mjema-3Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akiwa katika mkutano huo.

mama-mjema-4Mjema akisisitiza jambo kwenye hafla hiyo.

mama-mjema-5Picha ya pamoja kati ya ugeni kutoka China na viongozi wa Wilaya ya Ilala.

MANISPAA ya Jimbo la Xuzhou nchini China leo imefikia makubaliano na Wilaya ya Ilala ili kushiriki katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wilaya hiyo iliyo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yalifikiwa leo wakati Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alipokutana na ugeni kutoka China, Jimbo la Jiang Su, Manispaa ya Xuzhou ulioongozwa na Zhang Aijun ambapo walikubaliana kuindeleza Wilaya ya Ilala ili ifanane na maeneo mbalimbali ya China kwa kuzingatia usafi wa maeneo yake, kuimarisha usalama kwa kupeana ujuzi wa masuala ya kiusalama yanayotumiwa na wenzao nchini China. Hii ni pamoja na vifaa vya kisasa vya kudhibiti vitendo vya uhalifu na watu kulinda maeneo yao wanayoishi.

Masuala mengine ni kushirikiana na elimu hususani ya kisayansi na teknolojia ili kuchochea uanzishwaji na uendelezwaji wa viwanda nchini Tanzania kufuatana na malengo yaliyowekwa Rais John Magufuli ambapo pande zote zitatafuta maeneo ya kuwekeza katika nyanja hiyo.

Katika hatua nyingine, Mjema amesema katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, kimaendeleo China ilikuwa sawa na Tanzania, lakini nidhamu na bidii ya kufanya kazi ndivyo vimeifikisha ilipo, hivyo amewaomba Watanzania kuiga mfano huo huwa ili kufikia malengo ya mapinduzi ya kiuchumi.

 

RC MAKONDA AWAKARIBISHA WANA DAR KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU

Comments are closed.