The House of Favourite Newspapers

Manji Amcharukia Makonda Kutajwa Sakata la Madawa

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga na Diwani wa Kata ya Mbagala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Yusuf Manji amemcharukia Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kumtaja kama miongoni mwa watu 65 anaotaka kuonana nao katika Kituo Kikuu cha Polisi Ijumaa hii ili kufanya nao mahojiano kuhusu tuhuma za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Manji ameyasema haya leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar.
Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.
Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.
Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.
Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kituo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.
Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.
Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.
Manji: Mimi nitaenda kituo cha polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.
Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.
Manji: Nataka niwashitaki vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.
Manji: Kesho naenda polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.
Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.
Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.
Manji: Huwezi kuniita mimi kama ….. njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.
Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.
Manji: Kama unataka msaada omba msaada sio unaagiza msaada, unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?
Manji: Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilingi moja.
Manji: Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.
Manji: Hivi ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda kesho.
Manji: Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.
Manji: Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. “Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya” kesho namshitaki.
Manji: Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi. Nitakuwa namvunjia heshima.
Manji: Mimi sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.
Manji: Mkuu wa mkoa kunasehemu nimegongana naye Oysterbay na nIlienda kuonanana naye kama diwani wa Mbagala Kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka Mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama diwani siwezi kumuandikia rais. Alisema Manji.

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Comments are closed.