Kartra

Manji, Mo Uso Kwa Uso … Mchongo Mzima Upo Hivi

UPO uwezekano mkubwa wa wafanyabiashara na mabilionea hapa nchini, Yusuph Manji na Mohammed Dewji ‘Mo’ kukutana kwenye Dar es Salaam Dabi itakayopigwa Jumamosi hii.

 

Dabi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki, inatarajiwa kupigwa saa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni.

 

Mabilionea hao watakutana uwanjani kushuhudia mchezo huo ikiwa ni baada ya Manji juzi kutangaza rasmi kurejea ndani ya Yanga kuendelea kutoa ushirikiano.Kitendo cha Manji juzi Jumapili kuibukia kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana kwenye mkusanyiko mkubwa kama huo tangu alipotua hapa nchini mwezi uliopita, kimerudisha furaha klabuni hapo.

Katika mkutano wa juzi ambao Spoti Xtra lilikuwepo, mashabiki na wanachama wa Yanga walikuwa wakisikika wakisema kwamba, kuna uwezekano wakamuona tena Manji kwenye mchezo dhidi ya Simba kama alivyowafanyia sapraizi mkutanoni hapo.

 

Kama Manji ameweza kuja kwenye mkutano, basi hashindwi kuja uwanjani kushuhudia tukicheza dhidi ya Simba Jumamosi.“Uwepo wake naamini wachezaji watapata morali ya hali ya juu kwa sababu miaka ya nyuma alivyokuwa akifika uwanjani, wachezaji walikuwa wanapambana kweli,” walisikika wanachama hao wakijadili.

 

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa DYCCC, Chang’ombe, Dar, kundi la wanachama wa Yanga lilimfuata Manji na kumuomba kurejea mara baada ya mkutano huo kumalizika ambapo walimsindikiza hadi kwenye gari aliyokuja nayo.

 

Manji alithibitisha kuungana na klabu hiyo kwa ajili ya kuisapoti mbele ya safari akijaribu kushirikiana na viongozi waliopo ili kufikia mafanikio.

 

“Nashukuru nimerudi nyumbani. Kiasi nilichoacha Jangwani ni moyo wangu. Kwa hiyo naheshimu maoni yenu, nashukuru kwa kualikwa hapa leo (juzi), nawatakia kila la kheri na mbele ya safari nitajaribu kushiriki,” alisema Manji.

 

Wakati Manji akisubiriwa kwa hamu kuibukia uwanjani Jumamosi hii, Mo kama kawaida yake amekuwa akijitokeza katika michezo mbalimbali mikubwa ikiwemo ya dabi, hivyo huenda na yeye akawepo uwanjani hapo kushuhudia pambano hilo na wakakutana uso kwa uso.

Msimu huu, Mo alionekana katika baadhi ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba ilicheza dhidi ya Kaizer Chiefs, Al Ahly na AS Vita ambazo zote walishinda.

STORI NA WILBERT MOLANDI,Dar

RAIS KARIA APETA TFF | YANGA YAWEKA MKAKATI MZITO KUIUA SIMBA | KROSI DONGO…


Toa comment