Manula Azua Kizaazaa Simba, Kisa Mabao Ya Mbali

Aishi Manula

MLINDA mlango namba moja wa Simba, Aishi Manula, amezua kizaazaa klabuni hapo kutokana na rekodi yake mpya aliyoiweka hivi karibuni.

 

Rekodi hiyo si nyingine bali ni ile ya kuonekana kutokuwa vizuri kudaka mashuti ya mbali ambayo yamekuwa yakipigwa langoni kwake.

 

Katika mechi saba za Ligi Kuu Bara pamoja na moja ya Ngao ya Jamii ambayo Simba imecheza mpaka sasa, imefungwa mabao manne.

 

Matatu kati ya hayo, Manula amefungwa kwa kupigiwa mashuti ya mbali nje ya eneo la 18, bao la kwanza lilikuwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar, bao la pili na tatu ilikuwa kwenye mechi za ligi kuu dhidi ya Mwadui lakini pia hivi karibuni dhidi ya African Lyon.

 

Kutokana na hali hiyo, Manula anadaiwa kuzua kizaazaa ndani ya timu hiyo na anatakiwa kuhakikisha anakuwa makini na kuzingatia yale yote anayofundish­wa pindi anapokuwa uwanjani.

 

“Baada ya mechi ya Afri­can Lyon, Manula alikutana na viongozi wamemwambia kuwa rekodi zinaonyesha msimu huu mabao mengi aliyofungwa ni ya mbali yaani yaliyopigwa nje ya 18.

 

“Kwa hiyo anatakiwa kuwa makini anapokuwa uwanjani na kufanya yote anayo­fundishwa kama ambavyo anafanya vizuri mazoezini ili kuhakikisha hafungwi tena mabao kama hayo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Loading...

Toa comment