The House of Favourite Newspapers
gunners X

Manyanya Ahimiza Elimu kwa Watoto Wenye Mtindio wa Ubongo

0
Naibu Waziri Manyanya akiwapa zawadi ya juisi watoto hao.

 

Naibu Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amewahimiza wazazi wenye watoto walio na mtindio wa ubongo kuwapeleka watoto wao shule ili wakapate elimu huku akiwaonya wasiowapeleka watachukuliwa hatua za kisheria.

 

.. Akikagua bembea lililoharibika ambalo hutumiwa na watoto hao kwenye michezo yao.

 

Ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya Shule maalum ya Msingi Sinza na kujionea hali halisi ya kielimu ya wanafunzi wenye mtindio wa ubongo.

 

Akiwaasa wanafunzi hao.

 

Amesema wazazi wanapaswa kuthamini hasa watoto wenye mahitaji maalum kama walivyo watoto wengine wanaoanza shule kwa wakati mwafaka kiumri.

 

Manyanya akizungumza na wanafunzi wa Shule Maalum ya Sinza.

Pia amejionea baadhi ya changamoto zilizopo katika shule hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi huku akianza kwa kutoa pesa kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kutengeneza bembea zilizoharibika kwa ajili ya michezo ya wanafunzi hao.

Watoto hao wakifurahi na kuimba pamoja na Eng. Manyanya

 

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply