The House of Favourite Newspapers

MANYIKA AZIGONGANISHA SIMBA, AZAM FC

Kipa wa Singida United, Peter Manyika

IMETAJWA kuwa klabu za Simba na Azam FC zimeingia kwenye vita ya kusaka saini ya kipa wa Singida United, Peter Manyika ingawa kipa huyo amedai kuwa yeye bado ni mali halali ya Singida.

 

Taarifa za ndani zinadai kuwa Simba inampango wa kumsajili kipa huyo ilikuweza kuziba nafasi ya kipa Emmanuel Mseja, ambaye wana mpango wa kuachana naye ili kuongeza nguvu kutokana na majukumu ambayo wanayo msimu ujao.

 

Aidha inadaiwa wakati Simba ikifanya juhudi hizo nayo Azam hawako nyuma katika michakato yao ili kuweza kuhakikisha wanampata kipa huyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

“Taarifa zilizopo ni kwamba Simba na Azam kila moja kwa njia yake kwa sasa wamekuwa wakifanya jitihada ya kuweza kuhakikisha wanapata saini ya kipa huyo wa Singida United,”kilisema chanzo.

Championi lilimtafuta kipa huyo kuweza kupata ufafanuzi kuhusiana na suala la usajili wake na alisema:“Mimi taarifa hizo sina ndiyo nazisikia na bado nina mkataba na Singida kama kuna kitu ni bora mtafute meneja wangu atatoa ufafanuzi zaidi.”

Hata hivyo, Championi lilimtafuta meneja wa kipa huyo ambaye ni baba yake anayefahamika kwa jina la Manyika Peter, lakini hakuweza kupatikana.

Comments are closed.