The House of Favourite Newspapers

Maonesho ya Kuku Kutimua Vumbi Oktoba Mwezi Ujao

0
Dar es Salaam 27 Septemba 2024: Wadau wa Tansia  ya ndege wafugwao waliopo chini ya Taasisi ya Poultry Association  of Tanzania (PAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Nyama Tanzania  (TBM) wameandaa  maonesho  ya kimataifa ya ndege wafugwao yanayotarajia  kufanyika  Oktoba 18 na 19 mwaka huu Mlimani City jijini.
Akizungumza na Wanahabari, Sufia Zuberi kutoka Jumuiya  ya wazalishaji wa  vyakula vya mifupo Tanzani (TAFMA) amesema maonyesho hayo  ni ya nane  kufanyika ambapo yatakuwa ya kimataifa kwa maana yatakutanisha nchi mbalimbali.
“Tunategemea kupata wadau mbalimbali kutoka nchi tofauti duniani ikiwemo Ubelgiji, Ufaransa, Marekani, Uholanzi, China, India pamoja na Kenya na uzuri ni kwamba makampuni ya ndani yatashiriki kuweza kujifunza vitu mbalimbali kuhusu ufugaji” amesema Zuberi.
Ameongeza kuwa walengwa wa maonesho hayo watakuwa wadau wanaoshiriki katika mnyororo wa thamani wa ndege wafugwao ambao ni  watotoleshaji wa  vifaranga, wafugaji wa kuku wa nyama, wafugaji wa kuku wa mayai,  watengenezaji wa vyakula vya mifugo hususani vyakula vya kuku, wachakataji wa mazao yatokanayo na ndege wafugwao.
Ameeleza kuwa katika maonesho hayo hakutakuwa na kiingilio na yataambatana na utoaji  elimu kupitia semia zitakazofanyika kwa siku hizo mbili.
Kwa upande wake Katibu wa Chama za wadau wa uzalishaji wa vifaranga Tanzania (TCPA), Alpha Ibrahimu amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wafugaji wote Tanzania kuja kupata taarifa sahihi elimu na kujifunza maendeleo ya teknolojia yalikuwa kwenye sekta ya ufugaji.
“Hii fursa ambayo inakuja kwa mfugaji moja kwa moja ya kuweza kukutana na watu ambao watawapatia mahitaji yao katika ufungaji ikiwemo mayai, vifaranga na vifaa vinavyotumika katika ufugaji wakutane nao ili kama wanamaswali ya kuliza wanaweza kupata msaada kwenye maonesho hayo” amesema Ibrahim.
Ameongeza kuwa kwa nchi ya Tanzania matumizi  na ufugaji wa kuku na mayai  haupo kwa wingi sana hivyo maonesho hayo yatasaidia kuelimisha wananchi kuhusiana na ulaji wa kuku wa kisasa na mayai na kuwa hayana madhara yoyote.
Nae Grace Urassa,  Mkurugenzi  wa Audken Farm wazalishaji wa mayai amesema wao watakuwepo kwa ajili ya kulitangaza yai ambalo linasadia sana kuongeza wingi wa protini katika mwili na pia kuwaeleza watanzania kuwa bidhaa tunazozalisha Watanzania ni salama kwa mlaji na hazina madhara yoyote yale.
“Tunashirikiana na watu ambao tunafanya nao kazi na hivyo virutubisho tunavichukua kwao ni vitu ambavyo vinatusadia kuongeza virutubisho ambavyo vinachukuliwa vitu kama mchicha na nafaka nyingine zinatengenezwa kwa pamoja na kupata unga ambao ndio wanaopewa wale kuku wanaokaa ndani kufugwa kama virutubisho ukiachana na yule ambae virutubisho hivyo anajitafutia mwenyewe” amesema Urassa.
Kwa upande wake Lucy Masanga, mtaalam wa mifugo kutoka kampuni ya Thrischool Exim Limited amesema anawakaribisha wadau wote wa mifugo kushiriki katika maonyesho hayo kwani watajifunza na kupata elimu namna bora ya kufanya ufugaji wa kuku wa mayai na nyama.
Sambamba na maonesho hayo  kutakuwepo na semina za mada mbalimbali zinazohusiana na tasnia ya ndege wafugwao.
Maonesho haya yalianza mwaka 2015 Jijini Dar na mwaka huu 2024 yatakuwa Maonesho ya nane kufanyika.
Leave A Reply