The House of Favourite Newspapers

Maonesho ya Swahili International Tourism Expo 2015 yazinduliwa

0

1

Mgeni rasmi Dk. Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa maonesho hayo.
Maonesho haya ya pili ya Swahili International Tourism Expo 2015 yalipata nafasi ya kutembelewa na Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiwa ndiye mgeni rasmi pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania, Dk. Adelhelm Meru.
Maonesho haya yatakayochukua takribani siku tatu mpaka tarehe 03-10-2015 kwa mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, yalizinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza mwaka jana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ndiyo waandalizi wa maonesho haya.
2
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi akifanya mahojiano na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliofika katika tukio hilo la kipekee Tanzania.
3
                                  Mh. Gharib Bilal akiwa kwenye banda la Qatar.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania, Dk. Adelhelm Meru akiwa na Bi. Devotha Mdachi wa TTB.
6
Banda la KLM-Royal Dutch Airlines.
7
Mkurugenzi Mtendaji wa TTB akiwa na mgeni rasmi, Mhe. Gharib Bilal.
Leave A Reply