Maonyesho ya Tehama yaendelea Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta-Chang’ombe, Innocent Richard (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda lao.
Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Veta-Chang’ombe, Emmanuel Bukuku (kulia) akiwa kwenye banda lao akionesha kompyuta iitwayo ‘Computer Training Kit’ ambayo ni ya kisasa kwa ajili ya kufundishia.
Mwanahabari wa magazeti ya Raia Mwema, Ismail Mang’ola (kulia) akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa mmoja wa wasaidizi watoa huduma kutoka kampuni ya Digital Waves Africa Ltd, Patricia Bosco Komba, kwenye maonyesho hayo.
Patricia Bosco Komba wa Digital Waves Africa (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mteja aliyetembelea banda lao kujua huduma wanazozitoa.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye moja ya mabanda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia huduma zinazotolewa kwenye maonesho hayo.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye maonyesho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changanyikeni na mwalimu wao (katikati) wakiwa kwenye moja ya mabanda ya maonyesho hayo wakijisomea vitabu.
Hapa wanafunzi hao wakijisomea.
Juhudi za kujisomea zikiendelea.
MAONYESHO ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyoanza jana jijini Dar es Salaam, yameendelea leo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Maonyesho hayo ambayo yamevutia watu wengi, yanatarajiwa kumalizika tarehe 2 Oktoba.
Miongoni mwa waliotembelea maonyesho hayo ni pamoja na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Changanyikeni ya jijini Dar es Salaam.
NA DENIS MTIMA/GPL