Mapacha wa Obi Mikel, na mpenzi wake wafikisha miezi sita
John Obi Mikel akiwa na mpenzi wake pamoja na pacha wao.
MWANASOKA wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) John Obi Mikel na mpenzi wake, Olga, wamefurahia watoto wao mapacha wa kike kufikisha miezi sita tangu wazaliwe.
Watoto hao wanaendelea vyema kwa mujibu wa wazazi wao, Olga Diyachenko na Mikel, ambao walianza mapenzi motomoto mnamo mwaka 2013 walipokutana jijini London ambapo baba wa milionea wa Olga ana biashara mbalimbali.
Inasemekana pia msichana huyo ana uhusiano na mmiliki bilionea wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich.