Mapacha Watanzania Walioungana Watenganishwa Saudi Arabia

 

MAPACHA wa Tanzania walioungana, Anishia na Melanese, wametenganishwa nchini Saudi Arabia Desemba 23, 2018, na hali zao zinaendelea vizuri kwa wakati huu.

 

Jumanne Desemba 25, 2018 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha amethibitisha mapacha hao kutenganishwa.

 

Kwa mujibu wa gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette.com mapacha hao walitenganishwa na jopo la wataalamu 32 kwa muda wa saa 13.

 

Upasuaji huo uliofanyika katika hospitali ya Mfalme Abdullah, (King Abdullah Children’s Specialist Hospital) iliyopo katika mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.

 

Mapacha hao wa kike waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Missenyi, Kagera, Januari 2018,  walipofikishwa Saudi Arabia walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya kuona uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha.

 

 

Loading...

Toa comment