The House of Favourite Newspapers

MAPENZI KUNOGA KIPINDI CHA BARIDI NI TATIZO, SH’TUKA!

NI wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.

 

Mimi mzima na naen­delea vizuri katika ku­timiza majukumu yangu likiwemo hili la kuelimis­hana na kukumbusha juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi. Mpenzi msomaji wangu, nilishawahi kusema huko nyuma na leo naomba nirudie tena kwamba, mapenzi ya sasa yamejaa usanii wa hali ya juu.

 

Wapo ambao wanajua kupenda kweli na ukiwa naye utagundua hilo lakini kuna ambao uki­waangalia hata machoni tu utabaini wanapenda kiujanjaujanja. Yupo rafiki yangu ambaye alinipa mkasa wake ambao naona ni vyema na wewe ukausikia ili ujifunze kitu. Alini­ambia: “Faudhia alikuwa mpenzi wangu na nilikuwa na mpango wa kufunga naye ndoa. Kilichoniuma ni kwamba, alikuwa akinipen­dea pesa.

 

“Yaani akihitaji pesa, ili muendelee kuwa na amani ujitahidi kumpatia laa sivyo mtagombana au atakunu­nia hata wiki nzima. “Kwa hiyo kilichonifanya nimuache ni tabia yake ya kupenda pesa. Hata vile alivyokuwa ananiambia kuwa ananipenda nikagun­dua ni kwa sababu nilikuwa nampa pesa, pesa ikiwa haipo, haniiti baby wala mpenzi, huniita jina langu.

 

“Nilipofanya jaribio la ku­tompa pesa, alikata kamba. Hakunihitaji kabisa, nikajua kumbe alikuwa hanipendi mimi kama mimi bali pesa zangu.” Kupitia ushuhuda huu, nimejifunza jambo moja la msingi sana. Kwamba, in­awezekana wewe unasema mpenzi wako anakupenda kumbe ana sababu ya kukupenda.

 

Mimi nadhani ifike wakati ukae chini na kumfanyia tathimini mpenzi ili ujue kwa nini amekupenda. Hii itakusaidia sana kwenye maisha yako ya kila siku. Wakati ukilifanyia kazi hilo, naomba nizungumzie hii tabia ya baadhi ya watu kuwakumbuka sana na kujifanya wanawapenda sana wapenzi wao kipindi cha baridi.

 

Kwa watu wazima watakuwa wamenielewa namaanisha nini. Yupo dada mmoja ambaye na­fanya naye kazi, kila mvua ikinyesha akipita mbele za wanaume utamsikia akisema: “Bora mvua inyeshe ili tuheshimiane. Hapa anamaanisha kuwa, mvua ikinyesha mume ataona umuhimu wa mke, kinyume chake pia.

 

Wapo wanandoa wengi tu ambao huenda siku nzima walikuwa wamekorofishana lakini inapofika usiku na kile kibaridibaridi cha mvua, utaona tabasamu lin­afunguka. Baby…baby nyingii. Tofauti zao zinakwisha kwa sababu ya ile hali ya hewa.

 

Yupo msomaji wangu ambaye naye aliniambia kuwa, muda mrefu sana mpenzi wake amekuwa kama kamsusa vile. Akimpigia simu an­amwambia yuko bize. Cha ajabu katika siku za hivi karibuni mwanaume huyo amekuwa akihitaji kuonana naye kila siku.

 

Ak­iulizwa imekuwaje wala hana aibu ya kusema eti kibaridi kinamtesa. Sasa, kama mpenzi wako hakutafuti mpaka kibaridi ki­anze, au mvua inyeshe ndiyo anakutumia meseji nyingi nzuri na kuonesha anakupenda sana unadhani huyo ni mtu wa kuendelea kuwa naye? Tafakari na uchukue hatua

Stori: Amran Kaima- 0658 798 787

Comments are closed.