The House of Favourite Newspapers

Mapenzi yamnyoosha Amber Lulu

MWANADADA kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza sura kwenye video za Kibongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’, amesema kuwa mapenzi yamemnyoosha na kwa sasa ameamua kujiweka kando.

 

Amber, aliyewahi kuwa kwenye uhusiano na mastaa mbalimbali akiwemo staa wa muziki kutoka Kenya, Jackson Makini ‘ Prezzo’, alisema kuwa, amekuwa kwenye mahusiano mengi, lakini anaona ni kama anapoteza tu muda.

 

“Mapenzi yameninyoosha bora niyapige chini maana wanaume wengi wananipenda kwa sababu ya umaarufu wangu, lakini unakuta hawana mapenzi ya kweli kwangu. Ninaona tu huko ninapoteza muda na kuambulia maumivu, kwa hiyo bora nijiweke wazi tu, hakuna namna,” alimaliza

Stori: Neema Adrian

Comments are closed.