The House of Favourite Newspapers

Mapigano Makali Yazuka Mashariki mwa Ukraine, Hofu Yatanda Kulipuka Kinu cha Nyuklia

0

 

Mapigano makali bado yanaendelea Donbas

MAPIGANO makali yamezuka karibu na mji wa Pisky ulio Mashariki mwa nchi ya Ukraine, huku Urusi ikitaka kulitwaa eneo lote la viwanda la Donbas.

 

Afisa wa Urusi anayeungwa mkono na Jamuhuri ya watu Donetsk amesema kuwa Pisky imekuwa chini ya uthibiti wa vikosi vya Urusi. Lakini Maafisa wa Ukraine wamekanusha madai hayo na kusema kuwa vikosi vya Urusi vimeangushwa na Majeshi ya Ukraine.

Kumetokea uharibifu mkubwa wa miundombinu na majengo eneo la Donbas

Idara ya Kijasusi ya Uingereza, imeripoti kuwa Jeshi na viwanda vya Urusi vipo chini ya harakati kubwa, huku Moscow ikitafuta uwezekano wa Kusafirisha magari ya kivita na silaha nyingine za kivita ili kundeleza mapigano na Ukraine.

 

Kyiv imeishutumu Moscow kwa kufanya mashambulizi ya roketi, yaliyoua karibia raia 13 katika maeneo ya karibu na kinu cha nyuklia. Huku ikionya kuwa uthibiti wa Urusi katika kituo hicho cha nyuklia unahatarisha usalama wa eneo hilo.

 

 

Leave A Reply