The House of Favourite Newspapers

Mapigano Sudan: Mwigizaji Asia Abdelmajid Auawa Katika Mapigano Khartoum

0

Kifo cha mwigizaji maarufu, aliyefariki katika mapigano ya ufyatulianaji risasi kaskazini mwa mji wa Khartoum, kimewashitua wakazi wa mji huo huku wakisikia marafiki na jamaa zao wengi wakiuawa katika mapigano.

Asia Abdelmajid, ambaye alitimiza umri wa miaka 80 mwaka jana, alikuwa maarufu kwa maigizo yake – ambapo alipata umaarufu zaidi mwaka 1965 kwa mchezo wa maigizo uliojulikana kama Pamseeka.

Ulichezwa kwenye ukumbi wa maigizo katika mji wa Omdurman kuadhimisha mapinduzi ya kwanza ya Sudan dhidi ya kiongozi wa mapinduzi. Alifahamika kama mwanzilishi wa maigizo ya jukwaani – na mwigizaji wa kwanza aliyefanya maigizo ya jukwaani kama taaluma, baadaye alistaafu na kuwa mwalimu.

Familia yake ilisema kuwa alizikwa katika kipindi cha saa kadhaa baada ya kupigwa risasi Jumatano asubuhi kwenye uwanja wa shule ya chekechea ambako amekuwa akifanya kazi zaidi hivi karibuni. Ilikuwa ni hatari kumpeleka makaburini.

Haijajulikana ni nani aliyemuua kwa risasi katika makabiliano yaliyotokea katika kitongoji cha Bahri kilichopo kaskazini.

Lakini wapiganaji wa kikundi cha jeshi la dharura – Rapid Support Forces (RSF), ambao wameweka ngome zao katika maeneo ya makazi kote mjini humo, wanaendelea kupigana na jeshi, ambalo hufanya mashambulio kutoka angani.

Leave A Reply