Mapinduzi Sudan: Nyumba ya Waziri Mkuu Yazingrwa

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok amewekwa chini ya ulinzi nyumbani kwake baada ya Wanajeshi ambao hawajafahamika kuvamia makazi yake katika kile kinachotajwa kuwa ni jaribio la Mapinduzi ya Serikali, Mawaziri wengine wanne wanashikiliwa pia na Wanajeshi.

 

Vyombo vya habari vivimeripoti kwamba wanajeshi wasiotambulika wameizingira nyumba ya Waziri Mkuu huu. Runinga ya Al Hadath inaripoti kwamba wanajeshi wamewakamata mawaziri wanne na mwanachama mmoja wa serikali ya mpito.

 

Reuters pia imeripoti kwamba wanajeshi wamemia nyumba ya mshauri wa masuala ya habari wa waziri mkuu na kumkamata mapema Jumatatu.

 

Muungano wa Wataalamu nchini humo umewataka raia kuingia barabarani ili kufanya maandamano kwa lengo la kuzuia mapinduzi hayo ya kijeshi. Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na ripoti kuhusu kuzimwa kwa huduma ya mtandao nchini humo.

 

Viongozi wa kijeshina wa kiraia wamekuwa katika mzozo tangu walipoanza kugawana mamlaka katika serikali ya mpito baada ya mapinduzi miaka iliyopita mtawala wa kijeshi wam uda mrefu, Omar al-Bashir.

 

Serikali ya mpito-inayofahamika kama baraza huru -ililenga kutoa njia ya kufanyika kwa uchaguzi. Lakini hali ya wasi wasi imeendelea kuongezeka tangu mwezi Septemba, wakati jaribio la mapinduzi lililotekelezwa na wafuasi wa Bw Bashir kushindwa.

 

Siku ya Alhamisi wiki iliyopita, maelfu ya watu waliandamana kote nchini Sudan kuunga mkono demokrasia katika kipindi cha mpito. Lakini wafuasi wa jeshi waliwashutumu watawala wa kiraia kwa kutokuwa na ufanisi wa utendaji na kuporomosha uchumi wa nchi.


Toa comment